Important update: Healthcare facilities
CDC has updated select ways to operate healthcare systems effectively in response to COVID-19 vaccination. Learn more
UPDATE
Given new evidence on the B.1.617.2 (Delta) variant, CDC has updated the guidance for fully vaccinated people. CDC recommends universal indoor masking for all teachers, staff, students, and visitors to K-12 schools, regardless of vaccination status. Children should return to full-time in-person learning in the fall with layered prevention strategies in place.
UPDATE
The White House announced that vaccines will be required for international travelers coming into the United States, with an effective date of November 8, 2021. For purposes of entry into the United States, vaccines accepted will include FDA approved or authorized and WHO Emergency Use Listing vaccines. More information is available here.
UPDATE
Travel requirements to enter the United States are changing, starting November 8, 2021. More information is available here.

Kutoa msaada wa Kiroho na Kisaikososholojia kwa watu walio na COVID-19 Nyumbani (Mazingira yasiyo ya Kimarekani)

Kutoa msaada wa Kiroho na Kisaikososholojia kwa watu walio na COVID-19 Nyumbani (Mazingira yasiyo ya Kimarekani)

Watu wengi wanaougua au kupoteza mmoja wa familia wanahitaji kiongozi wao wa kiroho kutoa msaada wa kiroho. Wakati wa janga la COVID-19, njia salama zaidi ya kutoa msaada wa kiroho na kisaikolojia ni kwa simu, video, au kupitia majukwaa ya gumzo ya kibinafsi ya mitandao ya kijamii. Viongozi wa kiroho wanaweza kuomba, kushiriki mambo ya kiungu na ya kimaandiko na kushiriki ujumbe wa matumaini.

Ikiwa msaada wa kiroho wa ana kwa ana unahitajika, hati hii inatoa mwongozo ili utolewe kwa njia salama iwezekanavyo.

  • Dumisha umbali wa angalau mikono 2 (mita 2) kutoka kwa wengine, ikiwemo wakati wa kugawa
    chakula au maombi.
  • Vaa barakoa ili uzuie kuenea kwa COVID-19.
  • Chagua kufanya mikutano nje ambapo ni rahisi kuweka watu mbali kutoka kwa mmoja hadi mwingine na palipo na uingizaji bora wa hewa.

Ikiwa ni lazima uingie katika nyumba ya mtu aliye mgonjwa:

  • Nawa mikono kabla ya kuingia na baada ya kutoka katika nyumba hiyo; kwa ziara zinazochukua saa kadhaa nawa mikono mara kwa mara ukiwa kwenye nyumba hiyo.
    • Sugua mikono kwa sekunde 20 ili kuondoa viini hatari.
    • Ikiwa sabuni na maji havipatikani, unaweza kutumia kieuzi cha kutakasa mikono chenye alkoholi ya angalau asilimia 60. Kufanya hili kutakusaidia usiambukizwe wala kusambaza COVID-19 katika jamii.
  • Ukiwa nyumbani, fungua madirisha na milango ili kuwezesha hewa safi kuingia.
    • Usifungue milango na madirisha ikiwa kufanya hivyo kunahatarisha usalama au afya ya watoto au watu wa familia (mfano, hatari ya kuanguka au kuchochea dalili za ugonjwa wa pumu)

Tumia dakika chache kuzungumza na wengine nyumbani kuhusu vile wanavyoweza kupunguza hatari za kupata COVID-19. Wajulishe watu wa nyumbani kuwa mtu mwenye dalili hafifu nyumbani anaweza:

  • Kujitenga na watu wengine wa familia, iwapo inawezekana.
  • Ikiwa haiwezekani kujitenga na wengine kwa usalama, fuata mwongozo wa serikali kuhusu COVID-19, ikiwemo kuvaa barakoa ama kwenda katika kituo cha kujitenga cha jamii.

Wakati unatembelea familia:

  • Toa maneno ya faraja.
  • Ni bora kutomgusa mtu yeyote unapomwombea ili kuzuia hatari ya kuambukizwa au kusambaza COVID-19.
  • Ikiwa mtu mgonjwa katika familia ana shida ya kupumua, maumivu ya kifua au kuvurugika, mtu anapaswa kupiga simu kwa nambari ya dharura ya COVID -19, wasiliana na kliniki iliyo karibu au ita ambulansi.
  • Nawa mikono kabla ya kuondoka kwenye nyumba hiyo. Nawa mikono kabla na baada ya kuvua barakoa. Nawa mikono* kwa sekunde 20 kwa maji na sabuni au mchanganyo wa klorini iliyozimuliwa, au tumia kitakasa mikono kilicho na alkoholi ili kusaidia kuzuia kupata COVID-19 au kuisambaza katika jamii.

 

Orodha kaguzi ya vitu vya kutathmini au kuja navyo kabla ya kutembelea nyumba

  • Barakoa
  • Kitakasa mikono kilicho na alkoholi ya angalau asilimia 60
  • Tishu
  • Mkoba wa utunzaji wa nyumbani:*pdf icon Parasetamoli, glavu za matumizi ya mara moja tu, nguo ya kuosha, kadi yenye anwani, kiuwa viini, sabuni, barakoa
  • Orodha ya taarifa na habari za hivi karibuni za COVID-19 katika eneo (mfano, orodha ya vituo vya kujitenga)
  • Orodha ya huduma za msaada wa kijamii zilizopo (mfano, nambari ya simu ya maombi, mawasiliano ya barua pepe, kundi la kibinafsi la maombi kwenye mtandao wa kijamii)
  • Orodha ya hatua za kujikinga zinazopaswa kutiliwa mkazo ( tazama hapa chini)

Hatua za kujikinga zinazopaswa kutiliwa mkazo wakati wa ziara ya ana kwa ana

  • Kaa nyumbani ukiwa mgonjwa (isipokuwa unapohitaji huduma ya dharura kwa ajili ya tatizo la afya au huduma ya kimatibabu)
  • Vaa barakoa (barakoa isiyo ya kitabibu au kifuniko cha uso) ikiwa unatoka nyumbani kwako au huwezi kujitenga na wanafamilia wengine nyumbani.
  • Funika kikohozi na chafya kwa kutumia tishu au tumia upande wa ndani wa kiwiko chako. Tupa tishu katika pipa la taka haraka na unawe mikono
  • Nawa mikono mara kwa mara kwa maji na sabuni kwa angalau sekunde 20
  • Safisha na kuua viini katika sehemu zinazoguswa mara kwa mara nyumbani
  • Punguza kukaribiana na watu wengine kadiri iwezekanavyo nyumbani walio wagonjwa au walio na dalili
    (weka umbali wa angalau mikono 2 au mita 2) Mtu yeyote aliye mgonjwa au ambaye ameambukizwa anapaswa kujitenga na wengine kwa kukaa katika “chumba maalumu cha mgonjwa” au eneo (ikiwa kipo)
  • Unawajibika kusaidia kudumisha usalama wa jamii yako kwa kufuata hatua za kujikinga zinazopendekezwa:
    • Epuka kugusa uso wako kwa mikono ambayo haijaoshwa, hasa macho, pua, au mdomo
    • Jua na ushiriki tu ukweli kuhusu COVID-19 na usaidie kuzuia usambazaji wa uvumi na unyanyapaa katika jamii yako

Wasiliana na mamlaka ya afya ili kupata taarifa na mapendekezo kuhusu hatua za kijamii ambazo zimeundwa ili kukinga na kupunguza maambukizi ya COVID-19.